|
||||||
|
||||||
![]() |
||||||
| Sokoine University, Tanzania
Forest Health Centre, Ministry of Natural Resources, Kenya Tuskegee University, Alabama, USA U.S. Agency for International Development |
||||||
| 1.
Utangulizi Lengo la kupogoa miti ni kupata mimea yenye afya, nguvu, na ya kuvutia. Lengo hilo litafikiwa kwa kufuata taratibu za kupogoa, na kwa kuelewa namna gani, wakati gani, na sababu za kupogoa miti. |
![]() Kielelezo 1. Sababu za kupogoa |
2. Sababu Za
Kupogoa Sababu kubwa za kupogoa miti ya mapambo na miti ya vivuli ni kwa ajili ya usalama, afya ya miti, na kuifanya miti ipendeze. Zaidi ya hayo, kupogoa kunatumika kuleta mwamsho wa uzalishaji wa matunda na kuongeza ubora na thamani ya mbao. Kupogoa kwa ajili ya usalama (Kielelezo 1A) inahusisha kuondoa matawi ambayo yanaweza kuanguka na kusababisha madhara au kuharibu vitu na mali za watu, kupunguza matawi ambayo yanazuia kuona mbele kwenye barabara au njia ndogo za pembeni, na kuondoa matawi ambayo yanaingilia waya za umeme na simu. Kupogoa kwa ajili ya usalama kunaweza kuepukwa kwa kuchagua kwa makini aina ya miti (tree species) ambayo haitakuwa mikubwa kuliko eneo lililoachwa kwa ajili yao, na ambayo ni imara na ina umbo linaloendana na eneo hilo. Kupogoa kwa ajili ya afya ya miti (Kielelezo 1B) kunahusisha kuondoa matawi yaliyoshambuliwa na ugonjwa au wadudu waharibifu, kupunguza matawi ya taji ili kuruhusu hewa kupita kwa urahisi, na kuondoa matawi yaliyopishana na kusuguana. Kupogoa kunatumika kuimarisha umbile la ndani ya mti na kupunguza uwezekano wa mti kudhurika wakati wa hali mbaya ya hewa. Kuondoa matawi yaliyovunjika au yaliyoharibika kunafanya vidonda vipone haraka. Kupogoa kwa ajili ya kuufanya mti upendeze (Kielelezo 1C) inahusisha kuimarisha umbo na tabia ya mti, au kuamsha utoaji wa maua ya mti. Kupogoa kwa ajili ya kutengeneza umbo la mti (tree form) kunaweza kuwa muhimu hasa kwa mti uliokua kwenye eneo bila miti mingine karibu yake (open-grown tree) ambao ni mara chache hujipogoa yenyewe. |
| Mimea yote ya aina ya miti huangusha matawi kutokana na kuwa kwenye kivuli
na kwa kushindania mahitaji yao na mimea mingine kwenye eneo ilipoota. Matawi
yasiyoweza kujitengenezea chakula kwa njia ya kusanisi (photosynthesis)
hufa na kunyofoka, na vidonda vya matokeo haya huzibwa na nyama za kidonda
(woundwood). Matawi yaliyojishikiza vibaya kwenye mti yanaweza kuvunjwa
na upepo, theluji au barafu. Matawi yaliyotolewa kwa njia kama hizo mara nyingi
husababisha madonda makubwa na mara chache sana mandonda hayo hufunga. Kupogoa
kwa mpango maalumu kunaweza kutumika badala ya njia za asili ili kuongezea
uimara na urefu wa maisha ya mimea. Miti ina maumbo mengi, lakini ambayo ni ya kawaida ni umbo la pia (pyramidal, excurrent) au tufe (spherical, decurrent). Miti yenye mataji ya pia, mfano, miti mingi ya misindano (conifers) ina shina moja imara katikati na matawi yaliyokaa ulalo (horizontal) ambayo hayashidani na shina la mti. Miti yenye mataji ya umbo la tufe, mfano, miti mingi ya majani mapana (hardwoods), ina matawi ya ulalo (lateral branches) yanayoweza kushindana na shina. Kupunguza haja ya kupogoa ni vema kuacha mti katika umbo lake asili. Ni vigumu sana kupunguza matawi kwa njia isiyo ya asili bila kuhakikisha kufanya hivyo mara kwa mara. Pollarding na topiary ni njia maalumu za kupogoa ambazo hutumika kubadilisha umbo la asili la mti. Pollarding ni zoezi la kupunguza matawi kila mwaka ili kuondoa matawi yote mapya. Mwaka unaofuata, uvimbe wa matawi mapya hutokea mwishoni mwa matawi yaliyopogolewa. Topiary inahusisha kupogoa miti na vichaka kuwa na umbo la mnyama au vitu mbali mbali. Kama kukiwa na uangalifu wa kutosha, mti unaweza kupogolewa na kuwa na umbo lolote. Jinsi upogoaji mzuri unavyoimarisha umbo na tabia ya mti, upogoaji mbaya unaweza kuharibu hayo yote. |